Kama untaka kufanikiwa ni lazima ubadili
namna unavyowaza. Acha kuangalia
mshahara au kipato chako kidogo kama
kikwazo bali kama fursa. Usiangalie nalipwa
kidogo hivyo siwezi hili na lile bali angalia
kuwa nalipwa kaisi flani hiki kinaweza kuwa
kianzio cha kufanya moja, mbili, tatu. Hakuna
mshahara mdogo wala mkubwa bali kuna
matumizi mdaogo na makubwa, namna
unavyotumia kile unachokipata ndiyo itaamua
kile unachokiwekeza.
Kuna watu wanalipwa milioni tano kwa mwezi
lakini ikifika Tarehe 20 bado hawana hata
shilingi kumi na kamwe mishahara
haigongani, lakini kuna wtau wanalipwa laki
mbili lakini mishahara hugongana benki.
Badili fikra kuhusu kile unachokipata na
kukiona kama kianzio cha kufanya lolote.
Hata kama kinaweza kununua matufali mawili
tu jua kuwa ni mwanzo mzuri wa kujenga
nyumba, badili namna unavyowaza.makinspire.blogspot.com
![]() |
No comments:
Post a Comment