{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } MAPATO YASIYO NA KIKOMO,soma hapa kujua nini maana ya mapato yasiyo na kikomo ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

MAPATO YASIYO NA KIKOMO,soma hapa kujua nini maana ya mapato yasiyo na kikomo

Unapoongelea suala zima la mapato yasiyo
na kikomo ni sawa na wewe kufunga bomba la
maji mtoni, ili kuleta maji nyumbani kwako.
Maji yakishafika nyumbani wewe unayatumia
unavyotaka na hayakatiki. Wale wote
wasiofikiwa na mabomba ya maji majumbani
mwao, wao wanachokifanya ni kuchota maji
kwa kutumia vifaa kama ndoo, madumu n.k.
Watu hawa wakishapata maji, wanayatumia
na inafika wakati yanaisha. Mara tu maji
yanapoisha, inawabidi wafunge safari tena
kwenda kuchota maji popote yalipo, na
mzunguko unakuwa hivyo maisha yao yote.
Ukichota maji yanakuwepo nyumbani,
usipochota maji hayapo LAKINI yule mwenye
bomba anaendelea kupata maji masaa yote,
hata akiwa amesafiri maji yapo tu!.
Mfano huu wa maji ni sawa na mfumo wa
mapato tunayoyapata. Kwa maana nyingine ni
kwamba, wale wote tunaopata mapato hai au
mapato ya ajira (mshahara), tunafanana
kabisa na wale watu wanaochota maji mtoni
kila siku kwa kutumia ndoo, madumu n.k. Kwa
mfano: Mapato ya ajira -unalipwa siku
unapofanya kazi, usipofanya kazi haulipwi,
ukisafiri bila ruhusa haulipwi, ukiugua muda
mrefu hulipwi n.k.
Kwahiyo, mapato bila kikomo ni mapato
anayopata mtu pasipo kuwa na ulazima wa
kushughulika au kufanya kazi kwa wakati huo.
Mapato haya mara nyingi yanatokana na kazi
au shughuli uliyokwisha kufanyika kitambo na
kuendelea kupata mapato hayo “kimya kimya”,
kutokana na ukweli kwamba watu wengine
wanakuona tu umekaa lakini kumbe wewe
unaingiza pesa nyingi mfukoni.
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba mapato au
pesa isiyo na kikomo ni ile ambayo mtu
huipata mara kwa mara, lakini kwa kutumia
nguvu kidogo sana katika kuiendeleza. Mfano;
ni pesa itokanayo na haki miliki kama;k.m.
pesa ya mrahaba au “royalties” kutokana na
kuuza vitabu, album au kukodisha hakimiliki;
faida benki; kodi ya majengo au mashine; au
pesa kutoka kwenye biashara ambayo
haikuhitaji tena wewe kuwepo moja kwa moja
kama “biashara ya kupashana habari au
mtandao”. Hii ni mifano tu ya vyanzo vya pesa
isiyo na kikomo. Aina hii ya mapato
inapatikana baada yaw ewe kufanyakazi kwa
bidii sana kwa muda fulani (k.m. miaka 2
hadi 5), baadae unaendelea kupata pesa kwa
muda mrefu bila hata wewe mwenyewe
kushughulika tena au zaidi.
Uzuri wa mapato yasiyo na kikomo ni
kwamba, unaendelea kupata pesa kwa muda
mrefu baada ya kazi ya uzalishaji au ya awali
kukamilika. Hali hii ya wewe kupata pesa bila
kulazimika kufanya kazi tena ndiyo
ukuwezesha wewe kupata MUDA wa ziada na
hivyo kupata fursa ya kuwekeza muda huo
kwenye mambo mengine. Uzuri mwingine wa
mapato haya ni kwamba duniani kote
hayatozwi kodi kubwa kama mapato ya aina
nyingine
Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES