{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } HUKU NDIKO KUTAJIRIKA KWA KUPATA PESA NYINGI ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

HUKU NDIKO KUTAJIRIKA KWA KUPATA PESA NYINGI

Kupata pesa nyingi kunahitaji
ubunifu wa hali ya juu hasa katika masuala
ya uwekezaji. Ubunifu si kitu cha kutazamia
bali ni kitu ambacho lazima ufikiri kwanza
ndipo ukipate. Hali halisi ya maisha ni
kwamba, watu wengi hawapendi michakato
ya pesa inayowasumbua akiri zao. Matokeo
yake wanaishia kufanya michakato kama ile
inayofanywa na wengine wengi. Matokeo yake
nao wanapata pesa kama wenzao au pungufu
ya wenzao.
Unapofikia hatua ya kupokea pesa kama pesa
unakuwa umepokea “kazi iliyoisha” . Kwa
maana hiyo, uhitajiki tena kufuata mchakato
wa kusubili, kuvumilia, kulipa gaharama
kabla n.k, kama mwanzo. Ukiona watu
wanashangilia wanapopata pesa hasa
ambayo hawajaifanyia kazi, basi ujue kuwa
wanajisikia amani sana kwasababu,
wanakuwa wameepukana na kazi kama vile
kutenga muda, kulipa gharama kabla,
ubunifu, kuvumilia, kusubili n.k.
Kwakuwa pesa ni matokeo ya mchakato, ni
wazi kwamba kila mchakato una mwenyewe
na kwa maana hiyo, kila pesa ambayo haiko
mfukoni mwako ina mwenyewe. Kama wewe
ni mtu wa kufuata njia za mkato kila mara, ili
kupata pesa basi ujue kuwa kutajirika kwako
ni muujiza. Kwasababu, wale wote wenye
pesa zao watakuwa kama ukibahatika
wanakupa pesa kidogo sana na kwa muda
ambao wanajisikia kufanya hivyo bila kujali
shida zote ulizonazo.
Kwa upande mwingine, pesa unayopata kwa
kukwepa mchakato wa upatikanaji wake, ni
vigumu sana kubaki nayo, kwasababu pindi
unapoitumia ikaisha, huwezi tena kupata
pesa nyingine mara moja. Hii ni kutokana na
ukweli kwamba wewe unayepata pesa nje ya
mchakato wake unakuwa huna umiliki
wowote wa mchakato huo.
Unapoanzisha na kumiliki mchakato wa
kuzalisha pesa ni kwamba ikitumika ikaisha,
basi mchakato wako unaoumiliki unazaa tena
pesa nyingine. Kwahiyo, unaendelea kuvuna
pesa nyingi bila kikomo – Huku ndiko
kutajirika!
Tunahitaji kutambua kuwa matajiri wengi
duniani walianzisha na kusimamia michakato
ya kuleta pesa. Ndiyo maana wengine
pamoja na kwamba walishafariki, bado ile
michakato waliyoianzisha na kuijenga mpaka
leo inaendelea kutoa pesa.
Sasa imefika zamu yako kuanzisha na
kujenga michakato ya kudumu ya pesa. Na
huu ndio wakati muhafaka wa kujitoa kwenye
kundi la wapenda “pesa au mikate” ya bure.
Jijengee tabia kama ya matajiri ambao
upendelea zaidi michakato ya kuleta pesa
kuliko pesa yenyewe.

Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES