{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } NINI CHA KUFANYA USIPOONA MATUNDA YA KAZI UIFANYAYO ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

NINI CHA KUFANYA USIPOONA MATUNDA YA KAZI UIFANYAYO

Unakumbuka wakati unaanza kazi, kuna vitu
ambavyo ulitamani sana kuwa navyo,
ulitamani kuwa na chumba chako, angalau
chumba na sebule, kitanda, TV, kajiko ka gesi,
na vikorokocho vya ndani. Hembu angalia vile
vitu kama unavyo au huna na ulivipataje,
jiulize baada ya kuvipata pesa ya mshahara
uliyotumia kununua vile vitu iko wapi kama
sasa hivi huvinunui tena? Unajua ni kwanini
ulivipata hivyo vitu?
Huna haja ya kuumiza kichwa sana, ulivipata
kwakuwa ulikuwa na malengo na mtu
anapokuwa na mlengo flani basi moja kwa
moja huilazimisha akili yake kufanyakazi
kuelekea yale malengo. Kuna namna mbili za
kuweka malengo, namna ya kwanza ni kuweka
malengo bila kujijua “Unconscious Goals” aina
ya pili ni kuweka malengo ukiwa unajijua
“Conscious Goals”.
Aina hii ya kwanza ni ile ambayo kuna vitu
unapanga kuvifanya lakini si kwa mpangilio
au hukai chini ukasema haya ni malengo
yangu. Kama ambavyo ulisema unatamani
kununu TV na ukanunua hayo ni malengo
ambayo ulijiwekea, aina ya pili ni ile ambayo
unakaa chini na kuandika au kusema kabisa
mwaka huu nataka kufanya kitu A, B, Cna D.
Katika maisha mafanikio au vitu havidondoki
tu kama mvua ni lazima uviwaze na
kuviwekea malengo iwe ni kwa kujua kuwa
haya ni malengo au si malengo. Kwa watu
wengi ambao hawafanikiwa wanajikuta kuwa
badala ya kuweka malengo basi huweka
vikwazo. Kwamba kwa kuangalia mshahara
wako badala na kuuona mdogo badala ya
kuweka melango kutokana na mshahara wako
mdogo basi unajiweka vikwazo kutokana na
mshahara wako mdogo.
Hembu nifafanue kidogo, tuchukulia unapata
mshahara wa shilingi laki mbili kwa mwezi na
akiba ni shilingi elfu hamsini, kwa maana
kuwa hata ukijibana vipi utabakia na shilingi
elfu hamsini. Sasa umepata kiwanja cha
shilingi milioni moja, watu ambao
hawafanikiwi watawaza hivi “Mshahara wangu
mdogo siwezi kununua kiwanja cha milioni
moja”.
Lakini watu waliofanikiwa huweza hivi “Milioni
moja nikikusanya elfu hamsini hamsini, kwa
mwaka nitakuwa nalaki sita, hizi laki nne
zilizobaki kununua kiwanja ...ngoja niangalie
ofisini…siwezi pata mtu wa kunikopesha
kweli…hapa nikipunguza kupanda Bajaji…vipi
nikiwa napika mwenyewe si nita save…na
nikiuza na ile deki ya CD ambayo siitumiii…si
zitafika kweli…kuna na lile dili ofisini ngoja
ni….”
Umeona tofauti ya watu hawa wawili, yule
wakwanza baada tu ya kuona kuwa elfu
hamsini haitoshi kununua kiwanja cha milioni
moja alikaa kimya akasahau na
kujisahaulisha tena kuhusu kiwanja. Tena
utamsikia akisema “Sitaki kujipa tamaa za
bure, haya maisha ni lazima uridhike na
unachopata…” Lakini wapili yeye ataumiza
kichwa mpaka kupata anachokitaka, hivyo
ndivyo unavyotakiwa usiangalie usicho nacho
bali namna ya kupata cha kuongezea.makinspire.blogspot.com


Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES