{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } UMUHIMU WA KUWA NA MAALIFA KICHWANI KWAKO,jua umuhimu wa maalifa maishani kwako ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

UMUHIMU WA KUWA NA MAALIFA KICHWANI KWAKO,jua umuhimu wa maalifa maishani kwako


Kila maarifa yaliyopo kichwani ya kazi yake.
tumekuwa tukienda kuomba kazi na kufanya
usaili kwenye maofisi ya watu mbali mbali ili
mradi tupate ajira. Unapokwenda kwenye
usaili mara nyingi hauingii na hata karatasi,
lengo kubwa linakuwa ni kujua una uwezo na
maarifa kiasi gani kuhusu ulichokisoma na
kama unaweza kuleta tija kwenye kampuni
husika? Baada ya kufanya usaili wanaweza
kukuajiri na kukupangia kiasi fulani cha
malipo ambacho ndicho kinakuwa sawasawa
na thamani ya maarifa yako. Ndio maana
kuna viwango vya mishahara kazini. Ofisi
Nyingi mtu anapoenda kusoma akirudi
mshahara huongezeka, ni kwa sababu
ameongeza kiwango cha maarifa kichwani
mwake. Unapongeza maarifa mbalimbali
kichwani mwako na ya maisha ya kawaida ya
watu wengine ndivyo thamani yako Hupanda
kwa maana nyingine... Mshahara unaolipwa
na maarifa yako vinatosha na vinaendana
kabisa.
Tumekuwa kizazi kisichoweza kuhoji na
kuthibiti ujinga unaofanyika, kizazi
kisichoweza kijisimamia maamuzi. Kimekuwa
kizazi cha ndiyo kama yule alivyosema, ni
kizazi cha bendera fuata upepo. Ukisoma
biblia Wagaratia 3 mstari wa kwanza utaona
maandiko yanayoanza na kushangazwa kwa
kizazi kutokuwa na akili na nani alikiloga?
Familia nyingi zilizo bora kwenye maisha yetu
ya kila siku ni familia ambazo ziliwekeza
kwenye maarifa siku za nyuma kwenye maisha
yao ya kila siku. Mara nyingi tumepiga kelele
kuhusu swala la maendeleo na vitu
mbalimbali lakini tunashindwa kujiuliza je
watu walitumia muda gani kuwekeza katika
maarifa. Wahenga walisema, "Alivyo baba na
mama ndivyo watoto walivyo". Tumeendelea
kupiga kelele kwamba Tanzania kuna anguko
la elimu (maarifa), maana yake tumejua kuna
athari zake katika vizazi vijavyo. Unapokuwa
na maarifa zaidi ni rahisi kuwasaidia hata
watoto wako kwenye njia iliyo bora.
Usiwalaumu watoto wa kizazi hiki bila kujua
uwezo wa wazazi wao katika kuwekeza kwenye
suala zima la maarifa. Je wanatumia muda
gani na wanawekeza kiasi gani. Narudi
palepale. Maarifa ni jambo la urithi kwa
watoto kama ulivyo ujinga. Kama hautaki
watoto wako wawe wajinga siku zote wekeza
kwenye maarifa, nao watafaidi katika maisha
yao yajayo hata usipokuwepo.
Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES