{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } MAMBO MAZURI MUDA MWINGINE HUPITISHWA KWENYE NJIA MBAYA,soma hapa kujifunza mengi na update hamasa ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

MAMBO MAZURI MUDA MWINGINE HUPITISHWA KWENYE NJIA MBAYA,soma hapa kujifunza mengi na update hamasa


Hivi umewahi kumuona mdudu kiwavi, kiwavi
ni mdudu mwenye sura mbaya sana na
mwenye umbo baya sana, kwasababu
anapokuwa kwenye harakati za ukuaji
anakuwa kama mfano wa jongoo, lakini kitu
kimoja ambacho kinanishangaza kutoka
kwenye huyu mdudu ni kwamba ni yeye huyu
huyu ambae siku moja anakuja kuwa kipepeo,
najiuliza tu swali moja unadhani kwa kipindi
hajawa kipepeo angesema basi bora nife kama
ndo niko hivi,kipepeo angetokea?laa hasha
asingetokea, angesema mimi ndo nimeumbwa
hivi hivi na maisha yangu ndo haya haya
Mungu kanionea namatumaini leo
tusingeuona uzuri wa kipepeo.
Na maisha yetu ndivyo nalivyo muda
mwingine mambo mazuri huwa yanapita
kwenye matukio mabaya ambayo huenda
huyapendi, siku moja alikuepo jamaa mmoja
alikuwa amechoka kabisa kufanya kazi
ambayo anaifanya, huenda ni kama wewe
ulivyochoka kwenda kazini kwasababu
unaamka mapema sana, huyu bwana kila siku
akawa anamuomba Mungu apate kazi kubwa ,
nzuri na yenye mshahra zaidi ya ule ambao
alio nao kwasasa.lakini apate kazi
ambayoatakuwa na furaha, aliomba saana tu,
siku moja Mungu akajibu dua yake, alipewa
kazi na boss akachelewa kuiwasilisha
kampuni ikakosa tenda, basi kesho yake
alipofika kazini alikuta barua ya kufukuzwa
kazi.
Daaah jamaa alilia sana sana tu kwanini
amefukuzwa kazi, familia yake itaishije,
siunajua wafanyakazi huwa wakiwa kazini
wanakuwa wameridhika eee hawawazi hata
kufanyabiashara au mambo yanaweza
kuwaingizia kipato cha ziada kwa muda wa
ziada, basi alilia sana nakuanza kumlalamikia
Mungu kuwa amemuomba apate kazi sasa
ndo kafukuzwa kabisa.
Baada ya kuteseka kwa muda kidogo na
maisha kuwa magumu kwaajili ya kufukuzwa
kazi akapata muda wa kuwa anasoma
magazeti kupoteza mawazo, siku moja
akakuta gazeti kuna kampuni imeanzishwa
anatakiwa mfanyakazi mwenye sifa kama
zake, akaenda kufanya usaili akafanikiwa
kupata kazi, akapata cheo kama kile kile
alichoomba kwa Mungu, mshahara ule ule na
akawa free, sasa tujifunze kitu unadhani
aisingefukuzwa kazi angepata muda wa kukaa
kusoma gazeti na kupata habari iyo kiukweli
ingekuwa ngumu.
Rafiki usihuzunike unapokuwa kwenye wakati
mgumu, kwenye wakati ambao Mambo
hayaendi sawa, jua Mungu anakutafutia nafasi
iliyobora zaidi endelea kupambana hadi
kileweke, dhahabu ili ing'ae sharti ichomwe
moto, usikate tamaa usihuzunike siku moja
utakuja kuishi maisha yaliyo bora.
USIHUZUNIKE MDUDU KIWAVI, SIKU MOJA
UTAKUWA KIPEPEO
Asante kwa kutembelea na Endelea kutembele blog yako ya Maki inspire kwa elimu said I.
*@Mr motivation*
Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES