{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } WATANZANIA NA TABIA YA KULALAMIKA NA KULAUMU, soma hapa kujifunza mengi na kuacha tabia ya kulaumu na kulalamika ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

WATANZANIA NA TABIA YA KULALAMIKA NA KULAUMU, soma hapa kujifunza mengi na kuacha tabia ya kulaumu na kulalamika


Mbona unalalamika kila siku kwamba biashara yako ni ngumu? Kwani wewe ulianzisha biashara yako kwa lengo gani? Malalamiko kutoka kwa wajasiriamali imekuwa ni sehemu ya Maisha yao. Kila unapojaribu kuongea na wajasiriamali lazima usikie malalamiko mengi ikiwemo--
ukosefu wa mitaji ya kuendesha biashara.
Watu wanalalamika eti hawafikiriwi, hakuna anayewajali na hawasaidiwi! Yawezekana ni kweli, lakini kwa yeyote mwenye malalamiko na aketi chini na ajiulize hili; “Ndiyo hakuna anayenijali, hakuna anayenifikiria na hakuna anayenisaidia, kwahiyo…...”
Ukishajiuliza swali la “kwahiyo…” --bilashaka utaamua mojawapo kati ya haya:
ama ni kuacha kufanya biashara au kuendelea na biashara”. Endapo utaamua kuacha biashara kero na malalamiko yako yote vitakuwa vimeishia hapo na kimsingi utaweza kuendelea na maisha mengine.
Endapo utachagua kuendelea na biashara, maana yake ni kwamba matatizo unayolalamikia si makubwa kiasi cha kukuzuia kupata faida na pengine ndiyo maana umechagua kuendelea na biashara bila kujali matatizo na changamoto zilizopo.
Utamaduni wa kulalamika juu ya kazi tunazozifanya tumeurithi kutoka kwa watumishi hasa waajiriwa. Mfumo wa ajira duniani uko katika umbo la pembe tatu (piramidi). Ambapo unakuta mkubwa ni mmoja na chini yake kunakuwa na watu wengi kutegemea na ukubwa wa taasisi au kampuni husika iliyokuajiri. Mara nyingi watu walioko chini wakishindwa jambo lolote umsukumia yule aliyejuu ili afikiri na kutoa suruhisho kwaniaba ya wale wote anaowaongoza.
Kwa maana nyingine ni kwamba katika umbo hilo hapa juu, kuna mambo mengine huruhusiwi kuyafanya au kuyatolea maamuzi isipokuwa aliye juu yako. Pili, ukiwa mwajiriwa wa ngazi za chini kuna mambo ambayo yakikushinda unayapeleka kwa mkubwa wako kwaajili ya ufumbuzi zaidi.
Kwahiyo, chimbuko la tabia ya kulalamika ni utaratibu wa kutegemea maamuzi ya aliye juu yako. Kama anayepaswa kuamua jambo fulani, hafanyi hivyo kwa wakati au akafanya maamuzi vibaya basi utakuta waajiriwa walioko chini wanafanyakazi kwa kunung’unika muda wote, wanalalamika muda wote wanasema hovyo muda wote na hasa wakiwa maeneo ya nje ya ofisi zao.
Ikumbukwe kuwa, kinachowapa waajiriwa uhalali wa kulalamika ni ule mfumo au utaratibu wa ajira duniani ambao unatoa nafasi kwa mwajiriwa kuweza kupeleka malalamiko yake ngazi za juu endapo ataona kuna mambo ambayo hayaendi sawa.
Katika mfumo mzima wa ajira “MKUU” ni mtu wa mwisho na hatutarajii halalamike kwasababu hakuna mtu mwingine aliye juu yake ambaye anatakiwa kumpelekea malalamiko, ingawaje wengine ujikuta nao wakilalamika kwa watu wa chini yao. Wewe kama ni “Mkuu” kazi yako ni kuamua na kutenda basi!

*@Mr motivation*
Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES