Amini kwamba
unaweza kukipata au kuwa nacho kile
unachokihitaji.
Kuamini kabisa ndani yetu kuwa
tunauwezo wa kukipata au kuwanacho kile
tunachokihitaji ni sehemu ya kwanza na
muhimu katika kupata ujasiri. Habari
njema ni kwamba kila mmoja anauwezo.
Tunachokihitaji tu katika kuamini hili ni
kujikumbusha sisi wenyewe baadhi ya vitu
muhimu.
1. Wakati wowote wazia mafanikio
Najua yako mafanikio mengi umeshawahi
kuyapata kuanzia utoto wako. Yamkini
mengine yawezekana kuonekana kituko
lakini ukiyawaza sana na kulinganisha na
muda ule, utajua kweli kuwa yalikuwa ni
mafanikio makumbwa. Mfano vitu kama
kujifunza na kufanikiwa kutembea,
kufanikiwa kuzungumza, hata kwa lugha
ya kwenu. Kama wewe uliweza, wakati
kuna waliopata shida sana ili kuweza basi
bado unaweza kufanya mwakubwa zaidi.
2. Zipo nyakati utahitaji msaada wa
wengine
Katika yale yote unayodhani utayahitaji ili
ufanikiwe, usisahau kuwa utahitaji pia
msaada wa mtu au watu wengine. Na hapa
utafahamu kuwa hakuna hata mmoja
anayeweza kufanikiwa kwa kujitememea
mwenyewe. Hata ukijiangalia wewe kama
unajiona uliyefanikiwa, utajua wazi kuwa
kuna wengine ambao walikuwezesha kuwa
hapo ulipo kwa namna moja au nyingine.
Kwa kulitambua hili utaamini kuwa kwa
mafamikio yote ya mbeleni, wapo wengine
watakaolazimika kutubeba, kutushika
mkono na kutusaidia tufike kule tunakotaka
kufika
Home »
MOTIVATION AND INSPIRATION ISSUES
» AMINI INAWEZEKANA KWA NDOTO ULIYONAYO
No comments:
Post a Comment