Hapo zamani wakati watu walipokuwa na
mfumo wa biashara wa kubadilishana vitu
moja kwa moja (bartering system), uchumi
wa kaya ulikuwa imara sana, kwasababu kila
mmoja ilibidi afanye kazi ili kupata bidhaa.
Wakati huo, kulikuwa hakuna ujanja ujanja
na ilikuwa vigumu kwa mtu kumzurumu au
kuishi kwa rushwa kwani utaratibu ulikuwa ni
kwamba ili upate bidhaa fulani, ulitakiwa uwe
na bidhaa ya kwako. Jambo hili lililazimu
kila mmoja mwenye uwezo wa kufanya kazi
kuwajibika ipasavyo ndio aweze kuishi. Ni
bahati mbaya sana baada ya kuingia mfumo
wa pesa ambayo ukaa katikati ya muuzaji na
mnunuzi wa bidhaa, watu wengi tukasahau,
tukaanza kuweka nguvu na fikra nyingi
kwenye kutafuta hicho kitu cha katikati
“pesa” bila kukumbuka kuwa kitu ambacho
huwaleta pamoja watu hawa wawili yaani
muuzaji na mnunuzi, huwa siyo “pesa” bali ni
BIDHA
Home »
MOTIVATION AND INSPIRATION ISSUES
» MFUMO WA PESA UNAVYO WASUMBUA WENGI BILA KUUJUA VIZURI
No comments:
Post a Comment