{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } BILA SHAKA WENGI MNAMFAHAMU MWANAMZIKI HUYU WA KIMAREKANI ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

BILA SHAKA WENGI MNAMFAHAMU MWANAMZIKI HUYU WA KIMAREKANI



Bila shaka watu wengi mnamfahamu
mwanamuziki wa Kimarekani, Katy Perry lakini
inawezekana haufahamu kule alipotoka mpaka
kuwa hapo alipo kwa sasa.
Mwaka 1999, Perry aliamua kuachana na
shule na kujiingiza katika uimbaji. Asili yake
ilikuwa ni muimbaji wa nyimbo za injili,
aliyelelewa kiroho na wazazi wake waliokuwa
walokole kabisa.
Mwaka 2001, Katy Perry akazindua albamu
yake ya kwanza ya nyimbo za injili
aliyorekodia katika Studio ya Red Hill ambayo
haikuwa maarufu wala mafanikio. Baada ya
kuuza kopi 200 tu za albamu yake, studio
aliyoitumia ikaamua kufunga kwani haikuwa
na fedha.
Alichokifanya ni kubadilisha gia, akajitoa
kwenye muziki wa injili na kuingia kwenye
muziki wa kidunia ambapo akaelekea Los
Angeles na kurekodi na studio nyingine
iitwayo Glen Ballard.
Mwaka 2003, akaingia mkataba na Island Def
Jam kwa mkataba ambao baadaye ukafutwa.
Mwaka 2004 akasaini mkataba na Columbia
Records ambao walidhamiria kumfanya kuwa
kiongozi wa bendi yao ya The Matrix. Huko
hakukaa sana kwani napo wakaamua
kuachana naye.
Baada ya kutupwa na lebo tatu, usifikiri
kwamba Perry alikata tamaa, hakukata.
Aliendelea na muziki huku akifanya kazi
mpaka pale aliposaini mkataba na kampuni
ya Capitol Music Group mwaka 2006. Hapo
ndipo alipotoa ngoma kali iliyompa jina ya I
Kissed A Girl ambayo ndiyo iliyomuingiza
katika ulimwengu wa watu maarufu na pia
kumpa mkwanja wa maana.

Kwa nini wewe ukate tamaa kwa changamoto ndogo hizo, jipe moyo na endelea kutengeneza kesho yenye furaha na pesa nyingi.
Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES