{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } KAMA UNAONA UNAISHI MAISHA YA SHIDA, UMEPIGIKA, basi huyu bilionea anakuhusu ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

KAMA UNAONA UNAISHI MAISHA YA SHIDA, UMEPIGIKA, basi huyu bilionea anakuhusu

Kama unaona umeishi kwenye maisha ya
shida, kupigika basi hata huyu bilionea
mwanamke, Oprah Winfrey alikuwa hivyohivyo
na inawezekana Zaidi yako. Alizaliwa kwenye
familia masikini tu, alipokuwa na miaka tisa,
alibakwa mara tatu, yaani alibakwa na
mjomba, mpwa n ahata rafiki wa familia yao.
Alipofikisha miaka 14 tu, akapata mimba ila
alipojifungua, mtoto akafariki kwa bahati
mbaya.
Alipokuwa na miaka hiyohiyo, akapelekwa
kwenda kuishi na baba yake, Vernon huko
Tenessee nchini Marekani. Akajiweka zaidi
katika masomo yake, baadaye akajiunga na
Chuo cha Tennessee kusomea uandishi wa
habari. Akiwa hapo, akajiunga na redio fulani
ndogo ambapo huko akaanza kupata uzoefu
fulani.
Ingawa alikuwa kwenye hiyo redio ndogo,
mambo hayakwenda vizuri hivyo kufukuzwa
huku sababu ikiwa eti hakufiti katika
utangazaji. Baadaye akajiunga na kituo
kingine na kuwa mtangazaji katika kipindi cha
People Are Talking.
Mwaka 1983, akahamia Chicago kutangaza
kipindi kingine kiitwacho AM Chicago. Ndani
ya miezi michache tu, kipindi kikawa na jina
kubwa hata Zaidi ya kilichokuwa kikivuma
kipindi hicho cha Donahue. Hiyo ndiyo
iliyopelekea kipindi hicho kukiita The Oprah
Winfrey Show ambacho kiliendelea kusambaa
Marekani nzima na baadaye dunia nzima
kukifahamu.

Wakarubishe na wengine tuwe karibu, karibuni Sana
......nia ya makala
haya ni kujifunza na kutiana moyo kutokuta
tamaa
Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES