{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } HAYA NDIO MAZARA YA KUSEMA NA KUAMINI HUWEZI ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

HAYA NDIO MAZARA YA KUSEMA NA KUAMINI HUWEZI

Mtu anapoamini kwamba hawezi,
anayaambia mawazo yake ya kina
yamsaidie kumfanya ashindwe zaidi
kwenye kila jaribio analofanya. Badala ya
kufanya juhudi kujisaidia ili amudu,
hujipweteka kwa kuamini kwake kwamba
hata kama atafanya kitu gani, kamwe
hatamudu. Siyo rahisi kwa mtu mwenye
mawazo ya aina hii kuweza kufanikiwa
maishani.
Kuna watu ambao kwa sababu ya kukosa
kile ambacho jamii inakiona kuwa ndiyo
ufunguo wa mafanikio, huwa wanaamini
kwamba hawawezi kufanikiwa au kufanya
vizuri maishani kama hao ambao
wanacho. Kwa mfano, kwa kukosa elimu,
ujuzi au utaalamu fulani, watu wengine
hujihesabu kama wanyonge. Huchukulia
kwamba ni wale tu wenye elimu, ujuzi na
utaalamu fulani ndiyo wanaoweza au
wanaotakiwa kufanikiwa.
Bila shaka umeshawahi kusikia au hata
wewe mwenyewe kusema, “Si wamesoma
bwana’ ndiyo wanaojaliwa, sisi ambao
hatuna elimu kazi yetu itakuwa ni
kuwatumikia. Kauli kama hizi zina
chimbuko lake mbali sana, pengine katika
malezi yetu. Wazazi kwalizoea au
wamezoea kuwaambia watoto wao,
“Usiposoma kazi yako itakuwa ni
kuwabebea wenzako mizigo, unafikiri pesa
inaokotwa, nk. Kwa bahati mbaya mtoto
aliyelishwa “sumu” (‘EARLY CHILD
PROGRAMMING’) hii anaposhindwa shule,
huamini kwamba yeye atabaki
kuwatumikia wengine tu.
Tunapoamini kwamba kwa sababu hatuna
elimu ya kutosha na pengine ujuzi au
utaalamu fulani, hatuwezi kufika juu
kwenye mafanikio, tutakuwa tunatafuta
kufulia( ama vifafa vya kiuchumi)


Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES