Watu
wengi wanajivunia sana uzoefu, kiasi
kwamba wanaona ndio kitu pekee cha kuleta
mafanikio. Mtu akishajiaminisha tayari kuwa
ana uzoefu wa jambo fulani anakuwa mgumu
sana wa kupokea na kujifunza mambo mengi
mapya na wala haoni sababu hata kidogo ya
kufanya hivyo.
Kwasasa tutaendelea kushuhudia watu
wachache wakizidi kufanikiwa na kuwa
matajiri. Watu wengi wanaoamini katika
uzoefu walionao, bado wanaendelea kutumia
mbinu zile zile ambazo wamezitumia miaka
yote kutatua changamoto mpya.
Kutokana na kulewa sana “Uzoefu” mara
nyingi wamekuwa wagumu kupokea na
kujifunza mambo mapya. Ndiyo maana
kwasasa wapo watu wengi ambao wao
wamehapa kutokuijua Facebook achilia mbali
kuitumia – hayo yakiendelea, wale watu
ambao tuna uwezo wa kutengeneza picha
nzuri ya jambo ambalo halijatokea,
tunajitahidi kupokea na kujifunza mambo
mapya ambayo tunaamini ni mazuri.
Mfano; tayari watu wengine tunatafuta
masoko ya bidhaa na huduma mbalimbali
kupitia mitandao ya kijamii kama vile Face
Book (FB). Ebu fikiria mwenzako anatumia
FB kuwasiliana na wateja zaidi ya 1000 kwa
dakika, wakati wewe siku nzima inapita bila
hata kuwasiliana na mteja yeyote na wakati
huo huo pengine unazo bidhaa nzuri sana na
mpya
Home »
MOTIVATION AND INSPIRATION ISSUES
» HASARA ZA KUJIVUNIA NA KUTUMIA UZOEFU
No comments:
Post a Comment