Muda ni moja ya rasilimali ambayo ikipotea
hawezi kuirejesha na thamani yake ni kubwa
zaidi. Hakuna mtu anaweza kujua thamani
halisi ya muda mpaka muda utakapopea
ndipo unaweza kugundua. Kitendo cha wewe
kurudia rudia makosa waliyofanya
waliokutangulia ni moja wapo ya namna ya
kupoteza muda pasipokuwa na ulazima lakini
unapokaa na watu ambao wamekutangulia na
ambao wana uwezo mkubwa wa kupambanua
mambo ni rahisi kukueleza na kukusaidi
kutambua gharama za makosa ambayo
waliyafanya na ambayo wewe haupaswi
kuyarudia kuyafanya. Kuna namna mbili za
kujifunza kutoka kwa wengine , kwanza
tunajifunza kutokana na makosa
waliyoyafanya wao na pia tunajifunza
kutokana na mafanikio waliyoyafikia katika
kipindi cha uhai wao. Ni muhimu sana kukaa
chini na kuwasikiliza kwa kile ambacho
wanakueleza. “Mtu asiyewasikiliza
Walimtangulia,Kuna Wakati atalia na Asiwepo
Mtu Wa Kumfariji
No comments:
Post a Comment