{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } MAFANIKIO HAYATOKANI NA MIUJIZA ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

MAFANIKIO HAYATOKANI NA MIUJIZA

Mafanikio hayatokani na miujiza bali ni kitu
kinachojitokeza kutokana na mambo ya
msingi ambayo ni madogo madogo
yanayohitajika kupangwa na kufanyika kila
siku. Kwahiyo, tunaweza kusema kwamba,
mafanikio ni ujuzi au kusoma vitu vya
kawaida— lakini wakati mwingine tunahitaji
mtu fulani wa kutukumbusha na kutuonyesha
njia ambayo ni rahisi kufuata na kuweza
kufikia mafanikio tunayo yataka. Na hapa
nitaeleza umuhimu wa kuwa na mpango
mzuri kama hatua mojawapo ya kufuata ili
kuweza kufika kwenye mafanikio makubwa
kuliko unavyoweza kufikiri.
Kujenga maisha, kujenga kitu chochote kile,
ni kama kujenga nyumba; unahitaji kuwa na
mpango. Chukulia mfano, kama ungeanza
kubeba na kuanza kuweka matofari kwenye
msingi alafu akatokea mtu akakuuliza
“Unajenga kitu gani?” Je? Utaweka chini
matofari uliyobeba na kumwambia kuwa
hujui unacho jenga?” au utamwambia
unachotaka kujenga kuwa ni nyumba hata
kama bado haijajengwa. Mfano huu
unatufungua akili na kutufundisha kuwa,
mara zote“nyumba inaanza kujengwa mara tu
inapokuwa imekamilika” .
Tukirudi kwenye maisha tunaona kuwa
imekuwa vigumu sana kwa watu walio wengi
kuweza kuweka mipango madhubuti ya
maisha ya ndoto yao. Kwasababu ni ukweli
usiopingika kuwa wengi wetu hatujabainisha
kwa dhati kuwa uko mbeleni tunataka maisha
ya namna gani na kwakuwa hilo halipo katika
maandishi tumejikuta hatuna cha kupanga
kufanya kwa siku, wiki, mwezi, mwaka au
zaidi. Tunaamka asubuhi na kufanya
chochote kinachojitokeza kwenye akili na
fikra zetu. Kwa maana nyingine tumekuwa
watu wa kushughulikia mambo mapya na
matukio tu! Hii ni hatari na ni changamoto
kubwa sana iliyoko mbele yetu.
Kila mmoja wetu ambaye haliziki na maisha
aliyonayo kwa sasa, inabidi kujenga
utamaduni wa kuwa na nidhamu ya kufikiri
kwanza juu ya jambo ambalo unatarajia
kulifanya. Baada ya kufikiri, unahitaji
kuandika mawazo yako juu ya aina ya
maisha unayotamani kuyaishi miaka mitano,
kumi na zaidi ijayo, kwa kufanya hivyo
utakuwa tayari umekamilisha nyumba kabla
ya kuanza kujenga
Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES