{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } MWANZO NI MGUMU, msome huyu kijana wa kitanzania mwenye umri mdogo alifanikiwa kipesa ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

MWANZO NI MGUMU, msome huyu kijana wa kitanzania mwenye umri mdogo alifanikiwa kipesa

VIJANA wengi wamekuwa wakikimbia
kilimo vijijini wakidhani kuwa hakina faida
yoyote.
Hawafahamu kuwa siku zote mwanzo ni
mgumu kwani hata waliofanikiwa awali
walikuwa maskini na hawakuwahi
kufikiria kama watakuja kuwa matajiri
wakubwa duniani.
Kilimo na biashara ni miongoni mwa vitu
vilivyochangia utajiri wa watu wengi ndani
na nje ya nchi. Hata siku moja huwezi
kumiliki mabilioni ya fedha kwa kutegemea
kuajiriwa.
Katika makala haya kutana na
mfanyabiashara wa kwanza wa Kitanzania
kufanya biashara ya kusafirisha korosho
kwenda nchini Vietnam, Abbas Maziku
ambaye anaelezea alipoanzia, vikwazo
anavyokutana navyo, mafanikio na
matarajio yake kibiashara.
Maziku ni kijana wa Kitanzania aliyezaliwa
mwaka 1990 mkoani Mwanza.
Kitaaluma ni mtaalamu wa masuala ya
kibenki na fedha ambapo alipata Shahada
ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Zanzibar.
Baada ya kuhitimu masomo yake aliajiriwa
katika Benki ya Exim kama ofisa biashara.
Alidumu na kazi hiyo kwa muda mfupi na
kuamua kugeukia biashara ya mazao.
Alipoanzia
Akizungumza na mwandishi wa makala
haya, Maziku anasema alipoona kazi ya
kuajiriwa haina maslahi, aliamua kuanza
biashara ya kusafirisha mazao, hiyo
ilikuwa mwaka 2013.
Anasema alijikita katika biashara hiyo
baada ya kuvutiwa na mjomba yake
aliyekuwa akimiliki mashamba yenye
mazao mbalimbali.
Miongoni mwa mazao ambayo Maziku
alianza nayo na anendelea nayo mpaka sasa
ni korosho, ufuta, mbaazi, choroko, mtama,
alizeti, mashudu ya pamba na pilipili
manga.
Akizungumzia anapoyapata mazao hayo
anasema; “ninachofanya nakusanya mazao
kutoka kwa wafanyabiashara wadogo
wadogo ambao hukusanya mazao kwa
wakulima na katika minada inayofanywa
na vyama vya ushirika mkoani Lindi,
Mtwara, Dodoma, Singida, Shinyanga na
Tanga ambayo hufanyika mara moja kwa
kila wiki.”
Anasema baada ya hapo husafirisha mazao
hayo kutoka mikoani na kwenda
kuyahifadhi kwenye magahala
yanayotumika kuhifadhi mazao.
“Wakati wa kuyafungasha unapofika huwa
nawatumia vibarua na katika vifungashio
vyangu huwa na nembo inayoonyesha jina
la kampuni yangu.
Baada ya hapo sampuli hupelekwa katika
maabara za kupima ubora wa mazao
kimataifa iitwayo SGS,” anasema na
kuongeza:
“Mazao haya huwa nayasafirisha kwenda
nchini Vietnam kwa kutumia meli za
mashirika mbalimbali ikiwamo IPTL,
MAERSK na nyinginezo.”
Anabainisha kuwa huwa hatumii njia za
panya, hufuata hatua zote zinazohitajika
ikiwamo kupata kibali cha Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA), Wizara ya Kilimo
na Ufugaji, wanasheria pamoja na maofisa
wa usalama wa taifa ambao uhakikisha
hatua zote halali zimefuatwa.
Anasema biashara ya mazao kupeleka nje
ya nchi ina ushindani mkubwa hivyo
inahitaji umakini mkubwa ili kuweza
kujiendeleza, la sivyo unaweza kuishia
njiani kwa kupata hasara.
Anasema anakumbuka alianza na mtaji wa
Sh milioni mbili na sasa anazungumzia
mtaji wa Sh milioni 200.
“Si rahisi kufika nilipofikia, kwa sababu
biashara hii ina ushindani mkubwa.
Ninashindana na matajiri wakubwa wenye
uwezo wa kujipangia bei za mazao hivyo
ingawa nimepiga hatua lakini bado
ninahitaji kupanua biashara yangu zaidi na
zaidi,” anasema.
Anaeleza kuwa mwaka 2013 alipata hasara
ya mamilioni ya fedha baada ya ubora wa
mazao kupimwa na kuonekana upo kwenye
kiwango cha 48 badala ya 51 inayotakiwa,
hivyo alijikuta katika wakati mgumu kwa
kuwa
aliyumba kibaishara kutokana na mtaji
wake kukata.
Maziku anasema ilimlazimu kwenda
kukopa benki ili aendelee kufanya biashara.
“Nilipata hasara kubwa ambayo hadi leo
hii bado ninalipa deni nililokopa benki
ingawa pia fedha kutoka katika biashara
zingine inzozifanya zinaendelea kuifanya
biasahara hii kuendelea kuwapo,”anasema
mfanyabiashara huyo wa kimataifa.
Kila biashara haikosi vikwazo, Maziku
anataja vikwazo wanavyokumbana navyo
kuwa ni mtaji mdogo alionao.
Analia na ukiritimba unaofanywa na benki
mbalimbali ambazo ili kupata mkopo
wanahitaji dhamana kubwa kuliko uwezo
wa mfanyabiashara, jambo
linalokwamishaukuaji wa biashara.
Anataja kikwazo kingine kuwa ni
ukiritimba uliopo kwenye vyama vya
ushirika ambapo hupanga bei zisoendana
na ya soko la dunia.
Anasema hali hiyo inawafanya
wafanyabiashara wengi kushindwa kufikia
malengo.
“Wakati mwingine wafanyabiashara
wenzetu huturudisha nyuma kimaendeleo…
huwa tunawanunulia mazao kwa
makubaliaono ya kulipa baadaye, badala
yake hutoroka na fedha,” anasema.
Pamoja na mambo mengine, anataja
mafanikio aliyoyapata kupitia biashara
hiyo kuwa ni kumiliki kampuni mbili
ambazo ni GEFU Agromart Company
Limited na Lyone investment Company
Limited ambazo
zimeajiri wafanyakazi watano akiwamo
ofisa rasilimali watu, mhasibu, katibu
muhtasi, mwanasheria na meneja
mwendeshaji wa
shughuli za kampuni.
Mafanikio mengine ni kwamba ameweza
kujenga nyumba ya kuishi, kumiliki usafiri
na kupata fursa ya kusafiri kwenda nchi
mbalimbali kuhudhuria makongamano na
maonyesho ya biashara ya mazao, jambo
ambalo limemkutanisha na watu wengi
maarufu hivyo kujikuta akipanua wigo wa
biashara yake kimataifa.
Kwa sasa Maziku anatarajia kufungua
kampuni ya ujenzi ili kuweza kutoa ajira
kwa vijana wengi zaidi wa Kitanzania.
“Pia nina mpango wa kufungua kiwanda
cha kuzalisha juisi, mafuta ya alizeti,
mifuko ya plastiki na maji ya kunywa.
Kiwanda hiki nitakifungua kwa
kushirikiana na wawekezaji kutoka nje ili
nizidi kukuza uchumi wa Tanzania,”
anasema.
Anasema kwa kuwa ana uwezo wa kusaidia
jamii, haoni shida kutoa fedha zake
kuwasaidia wasiojiweza wakiwemo yatima.
“Kidogo nilicho nacho huwa nakitoa na
kwa wenye mahitaji maalumu lakini huwa
sipendi kujitangaza,” anasema
mfanyabiashara huyo.
Maziku anawashauri vijana wenzake kuwa
na uthubutu kama aliokuwa nao yeye,
aliiona fursa akaichangamkia na hadi sasa
amefikia
katika hatua nzuri.
“Vijana tusibweteke, vikwazo ni vingi lakini
hatupaswi kukata tama. Hata
waliofanikiwa kama akina Mo Dewji
hawakuanzia juu. Walipambana na uzuri ni
kwamba wafanyabiasahara wakubwa kama
Mo si wachoyo, huwa wanajitoa kusaidia
wengine kwa kuwapa ushauri wa
kibiasahara
Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES