Mtu yeyote anapoingia katika maisha
huwa anakabiliwa na changamoto ya
kuamua kati ya kujiajiri au kuajiriwa.
Kuajiriwa kunakuhakikishia usalama
kazini japokuwa usalama huo siku hizi ni
nadra sana kuwepo, wakati kujiajiri
hukuhakimkishia uhuru wa kuamua
mambo yako. Watu wengi huamua
kuchagua kuajiriwa kwa sababu ni rahisi
kuliko kuwa wajasiriamali ambako ni
kugumu, tatizo wanalolipata ni kuwa
wanaishi kwa kutegemea mshahara
ambao huwa hautoshi na kujiingiza
kwenye madeni mabaya ambapo hukopa
kwa ajili ya matumizi na kuendelea kuwa
na madeni makubwa zaidi. Kukopa siyo
kubaya ila kuna madeni mabaya na
madeni mazuri madeni mabaya ni yale
ambayo mtu anakopa kwa ajili ya hela ya
kula au kutumia, madeni mazuri ni yale
ambayo mtu anakopa kwa ajili ya
kuwekeza kwenye vitegauchumi au
kwenye biashara kwa kufanya hivyo mtu
anaweza kujitoa kwenye matatizo.
Wengine wanapata mishahara mikubwa
lakini wanashindwa kutumia pesa zao
vizuri kwa kujiingiza kwenye maisha ya
anasa na kuwa kwenye madeni makubwa.
Kwa mfano unaweza kukuta mtu
amenunua magari manne ya kutembelea
wakati ambapo angeweza kuwa na gari
moja na akawekeza kwenye kujenga
nyumba za kupangisha na kuweza
kujiingizia kipato. Uamuzi wa kuajiriwa
ni sawa na kuwa kifungoni hupaswi
kuishi katika hali hii unahitaji kuwa
huru. Njia ya kujinasua katika tatizo hili
fanya yafuatayo; wakati uko kazini
ukiwa umeajiriwa unaweza kuanza
kufanya juhudi za kujikwamua kwa
kuanzisha miradi midogo midogo au
kujishughulisha na kuwekeza kwenye
vitegauchumi pesa zako ili ziweze
kukusaidia baadaye
No comments:
Post a Comment