Home »
MOTIVATION AND INSPIRATION ISSUES
» UNAFANYA NINI UNAPOFIKWA NA WAKATI MGUMU MAISHANI, fanya haya wala usilalamike na kulaumu
UNAFANYA NINI UNAPOFIKWA NA WAKATI MGUMU MAISHANI, fanya haya wala usilalamike na kulaumu
Inapofika wakati unakutana na magumu
mengi sana katika maisha,ndiyo wakati sahihi
zaidi unapoanza kulaumu; unalaumu labda
kwa nini umezaliwa na wazazi maskini,kwanini
umezaliwa mweusi,kwanini umezaliwa mkoani
na siyo Dar es salaam,au kwanini umezaliwa
Dar es salaam lakini maeneo kama Tandale au
Tandika na sio maeneo kama Msasani na
Masaki…kwanini umesoma shule ambazo
unaamini ni mbaya na siyo zile zenye skuli
bus,unalaumu unalaumu!
Kila siku umekuwa mtu wa kulaumu na
kujilaumu,kila nukta ni nukta inayoondoka na
majuto;kujuta kwanini mimi? Kwanini mimi?
Niksize wewe mdogo angu unaenisoma,ewe
mkubwa wangu unaenisoma na yeyote yule
unaenisoma sasa,DUNIANI UPO PEKE AKO!
Mama yako,baba yako,mjomba ako,shangazi
yako nae yupo peke ake,kila mtu yupo peke
ake ,kwa kingeleza ningesema YOUR NOT
ATTACHED TO ANYONE ,sasa fahamu ilo,ishi
ukiwa unafahamu ilo,ulizaliwa katika familia
duni ,huo uduni ni wa familia yako sio
wako,ulisoma katika shule duni,huo uduni wa
shule sio wako,ulishinda na njaa,io njaa ni
mapokeo,sio yako,ujui ufanye nini upate
unachohitaji? Kutokujua sio kinga wala dawa
ya kukosa unachohitaji, endelea kupambana usikate tamaana ww ni mshindi ishi ukitambua hilo ndugu yangu, wengi walipitia hayo sio we we tu ila walipambana hivi sasa wana mafanikio makubwa sana, kwako pia inawezekana.
No comments:
Post a Comment