{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } PANDA MBEGU YA UJASIRI KWA WALIO CHINI YAKO ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

PANDA MBEGU YA UJASIRI KWA WALIO CHINI YAKO

Naona ni
vema  kujifunza jinsi ya sisi
kuwa msaada kwa walioko chini yetu
katika kuwajengea ujasiri. Kama
nilivyogusia awali, wengi wetu hawana
ujasiri leo kwa jinsi mazingira ya makuzi
yao yalivyokuwa. Wapo walio wahi
kunyanyasika na kunyimwa fursa za
kusema kitu mbele ya watu wazima, wako
waliokuwa wanapingwa katika chochote
kile walichowahi kukiongea. Sio kupingwa
tu, nafahamu pia wako waliokuwa
wanapokea kipigo baada ya kujaribu kitu
na bahati mbaya wakakosea kidogo. Watoto
hawa walitendewa haya katika mazingira
ya mashuleni au hata manyumbani, hapa
namaanisha walifanyiwa haya na walimu
au hata wazazi au walezi wao pasipo kujua
kuwa walikuwa wanapanda mbegu ya kuua
ujasiri katika maisha mazima ya utu uzima
wa watoto hao.
Yamkini wewe ni mzazi, kila unaporudi
nyumbani unamwona motto wako
anabadilika, anaogopa kukaa nawewe au
kusema na wewe kitu chochote wakati hana
kosa lolote, usinyamaze kimya, labda kuna
mazingira anayoishi na kukuzwa akiwa
shuleni yanayo muharibu taratibu. Yamkini
pia wewe ni mwalimu na unamshangaa
mtoto fulani jinsi alivyo muoga,
anayejificha nyuma ya wenzake na
asiyejaribu chochote, katika hili hutakiwi
kunyamaza kimya, labda kuna maisha
motto huyu anayaishi na kukuzwa
nyumbani ambayo yanaharibu utu na
ujasiri wake.
Bahati mbaya athari za makuzi haya
hazionekani kwa dhahiri sana mtoto awapo
mdogo, bali yeye mwenyewe anapokuwa
mkubwa anajishangaa yuko tofauti na
wengine. Lile analolitamani kulifanya au
kuliongea anajikuta hawezi kwasababu
hana ujasiri hata chembe. Kila ndoto
aliyowahi kuwanayo awali inafifia taratibu
na mwisho ina kufa. Katika mazingira haya
wakulaumiwa ni wazazi, walezi au
wanaotoa makuzi mashuleni. Wito wangu
kwa sisi wote ambao tunazungukwa na
jamii ya watoto ni kwamba tujitahidi sana
kuthamini ilembegu ya ujasiri ambayo
watoto wanaotuzunguka wamezaliwa nayo.
Iwe ni watoto wetu au wawenzetu, sote
tunawajibika kukuza na kuendeleza chembe
ya ujasiri ambayo watoto hawa wanayo ili
waweze kuiona kesho yao yenye mafanikio
makubwa. Mimi nimepata nafasi maranyingi
sana ya kuzungumza na vijana wakubwa
au watu wazima wengi ambao wamekuja
kufahamu wakiwa watu wazima kuwa
chanzo cha wao kutokuwa na ujasiri ni
makuzi waliyopokea kwa wazazi wao. Watu
hawa wengi wao wameendeleza chuki
kubwa sana na wazazi wao kwavile
wamekuwa wakijitazama kama
waliodhulumiwa kitu muhimu sana
maishani. Wako walioweza kusamehe
ingawa kwamaumivu makubwa sana.
Badala ya kuwa wakala wa kuua ujasiri wa
walewadogo wanaotuzunguka tuwe
mawakala wazuri wa kukuza na kujenga
ujasiri wao.

Asante

Share:

Related Posts:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES