Watu wengi wanashindwa kuwa na ufanisi kwa
sababu ya matumizi mabaya ya muda. Hata
hivyo kila binadamu ana masaa 24, siku 7 kila
wiki na miezi 12 kwa mwaka. Tafiti za
matumizi ya muda zinaonyesha ni watu
wachache sana wanatumia nusu ya muda wao
wa kazi kuzalisha na kwa sababu ya matumizi
mabaya ya muda wenginge wanakosa hata
muda wa familia zao. Ili kutumia muda wako
vizuri ni vema ukatambua mambo yafuatayo.
1. Mambo yanayoiba muda wako: Muda
unapotea kwenye vitu vingi ambavyo sio vya
lazima kwa wakati fulani. Kwa mfano
matumizi ya simu yasiokuwa na utaratibu,
social media (whatsapp, instragram, face book
n.k), watu wanokutembelea bila taarifa,
kukosa mpango wa siku, kushindwa kufanya
maamuzi, mikutano isiyo ya lazima, sherehe,
kutaka kufanya mambo mengi wakati mmoja,
siasa, n.k
2. Ili kuongeza ufanisi katika kutumia muda
wako hakikisha
• Panga kazi zako kwa umuhimu
(prioritization)- yapo mambo membi ya
kufanya lakini chagua yale ya msingi. Kila
unapopanga jambo jiulize je ni muhimu?
Linaniongezea nini katika biashara, kazi,
familia au jamii yangu?
• Andaa mpango wako wa kazi kila siku (to do
list)- unataka kufanya nini na wakati gani?
usikose diary yako au mahali utaandika vitu
unataka kufanya. Kila siku jioni panga
utafanya nini kesho yake na baada ya kazi tiki
mambo uliyofanya na yaliyobaki.
• Jifunze kusema hapana. sifa kubwa ya watu
wenye mafanikio ni kusema “hapana”- “ability
to say no”. Usifuate mkumbo fanya vitu
ulivyopanga.
• Jipangie muda wa emergence na vitu
ambavyo hukutarajia.muda huu unaweza
kuupa asilimia 10 ya muda wako. Mambo
mengine yapangie muda kabla.
• panga ajenda ya mikutano yako hata kama
unaenda kukutana na mtu uwe na ajenda.
Baada ya hapo aga endelea na kazi zako.
• Fanya maamuzi kwa haraka na uwe mtu wa
vitendo “be an action oriented person”.
Maneno yasiyokuwa na vitendo ni siasa na
hayaleti matokeo. “Ukisema kitu na
hukikifanya, tambua unafanya siasa badala ya
kazi”
Home »
MOTIVATION AND INSPIRATION ISSUES
» TUNZA MUDA WAKO KUONGEZA UFANISI WA MAFANIKIO
No comments:
Post a Comment