 |
Abraham Lincoln hakukata tamaa kamwe,kwanini wewe ukate tamaa?! Alizaliwa katika umaskini, Lincoln alikuwa mara nyingi anakabiliwa na kushindwa katika maisha yake. Alipoteza uchaguzi mara 8, mara 2 alishindwa katika biashara na akakumbwa na ugonjwa wa kuvunjika neva! Angeweza kukata tamaa mara nyingi - lakini hakufanya hivyo, na kwa sababu hakukata tamaa,akawa mmoja wa marais wakubwa katika historia ya Marekani! Hii ni njia aliyopitia Lincoln kufika White House: 1816 Familia yake ililazimishwa kutoka nyumbani kwao.Ilibidi Lincoln afanye kazi ili kuwasaidia. 1818 Mama yake alifariki. 1831 Alishindwa katika biashara. 1832 Aligombea ubunge-akashindwa 1832 Pia alipoteza kazi yake - alitaka kwenda shule ya sheria lakini hakuchaguliwa. 1833 Alikopa fedha kutoka kwa rafiki yake ili kuanzisha biashara lakini ilipofika mwisho wa mwaka alikuwa amefilisika.Alitumia miaka 17 iliyofuata ya maisha yake kulipa deni hili! 1834 Aligombea ubunge tena - akashindwa. 1835 Aliingia kwenye uchumba ili afunge ndoa,mchumba wake alifariki na moyo wake ulivunjika sana. 1836 Alikumbwa na ugonjwa wa kuvunjika neva na alikuwa kitandani kwa miezi sita. 1838 Aliwania kuwa msemaji wa bunge - akashindwa. 1840 Aliwania kuwa mchaguzi - akashindwa. 1843 Aliwania Congress - akashindwa. 1846 Aliwania Congress tena - wakati huu yeye alishinda - alikwenda Washington na alifanya kazi nzuri. 1848 Aliwania kuchaguliwa tena Congress - akashindwa. 1849 Aliwania kazi ya uafisa ardhi jimboni kwake - akakataliwa. 1854 Aliwania kuwa Seneta - akashindwa. 1856 Aliwania uteuzi wa kuwa Makamu wa Rais kupitia chama chake kitaifa - alipata kura chini ya 100 na kushindwa. 1858 Aliwania kuwa Seneta tena - akashindwa. 1860 ALICHAGULIWA KUWA RAISI WA 16 WA MAREKANI!!
Yote yanawezekana pambana usikate tamaa |
No comments:
Post a Comment