{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } PESA ZAKO ZINAENDA WAPI ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

PESA ZAKO ZINAENDA WAPI

Pesa Zako Zinaenda Wapi?
Hili ni swali ambalo karibu kila mfanyakazi
hujiuliza hasa wale ambao hawanywi pombe
au si watu wa kuhonga, hawana matumizi ya
anasa ya kuonekana. Kwa wafanyakazi wengi
bila kujali matumizi yao yakoje hujikuta
mwisho wa mwezi hawana kitu na husubiria
mishahara kwa hamu. Angalau wale watu wa
anasa wanajua pesa zao zinaenda wapi?
Kabla ya kukuambia pesa zako zinapoenda
kwanza ingekuwa vyema ukafahamu
“Matumizi ya anasa ni nini?”. Kwa watu wengi
matumizi ya anasa ni kununua vitu vya bei
ghali kama vile nguo za gharama, magari,
kunywa pombe, kuhonga sana na vitu kama
hivyo vya kistarehe na hii ndiyo maana watu
ambao hawafanyi hivyo vitu hujiona kama
hawafanyi anasa huku pesa zikiwa
hazionekani.
Lakini hiyo siyo kweli, tafsiri halisi ya
matumizi ya anasa (Kwa mujibu wangu) ni
matumizi yasiyo na msingi wala ulazima
wowote. Kwa maana ya kwamba aina ya
matumizi yote ambayo kama usingeyafanya
yasingeathiri afya yako, heshima yako mbele
ya jamii na huwa hayabadilishi chochote
kama yakifanyika.
Kwa tafsiri hii kuna mambo mengi ambayo
tunayafanya ambayo si ya msingi na hutumia
pesa nyingi bila sisi kujijua, kwa mfano
kununua mashati kumi wakati unavaa
matano, kununua pea 20 za viatu wakati
unavaa tatu tu, kuwa na simu mbili za
smartphone wakati unatumia moja tu kwenye
mtandao, kunywa soda kila baada ya mlo
wakati maji yangetosha, kupanda Bajaji
wakati daladala zipo au ungetembea kwa
miguu ungeimarisha afya yako.
Kuwa na aina tano za pafyum wakati moja
ingetosha, kununua TV ya nchi 40 wakati ya
21 ingetosha, kutoa michango ya haruisi kila
unapopewa kadi, michango ya birthday party,
kushona sare na suti kila harusi, kununua
nguo mpya kila tukio linapotokea wakati
unazo ndani na mambo mengine madogo
madogo ambayo unayafanya mara moja moja
lakini ukikaa chini na kujumlisha unakuta una
mtaji wa duka kubwa la nguo au ungekuwa
ushanunua kiwanja.
Haya mambo hatuyaoni kuwa ni ya anasa
kwakua hatuyafanyi kila siku na kwakuwa
jamii inayaona kama mambo ya kawaida,
lakini kiuhalisia ni mambo ya anasa, tena ya
anasa kuliko hata kunywa pombe. Unaishi
msela au dada mwenyewe una sahani kumi,
vikombe 20 na vitu kama hivyo ambavyo
vimekaa kupamba kabati then what baada ya
kupambika?
Vitu hivi vinaweza kuonekana vitu vya
kawaida, muhimu kuvifanya lakini si kwa mtu
ambaye ndiyo kwanza anaanza ajira, huna
hata kiwanja au sehemu yoyote uliyowekeza.
Katika umri flani na kwa kuangalia kipato
chako, kuna mambo ambayo ili kufanikiwa ni
lazima kuyapunguza au kuachana nayo
kabisa kwani kwa kuyafanya hayakuongezei
chochote na hukupunguzia pesa.
Vitu vyote hivi au aina hii ya matumizi
wazungu huita ‘Liability” Ni vitu ambavyo
havizalishi bali huhitaji kutumia pesa kila
siku. Unapaswa kuwa na “Asset” kwa manaa
ya kitu ambacho kitazalisha au kinapanda
thamani bila kuhitaji kutumia pesa ya
mfukoni. Naamini mpaka hapa umeshajua
pesa zako zinaenda wapi na uko tayari kwa
kujua ni kitu gani cha kufanya?
Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES