{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } USUKATE TAMAA, PAMBANA ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

USUKATE TAMAA, PAMBANA

 Nilisoma historia
ya mwanasayansi mmoja Thomas Edson
ambaye ndiye aliyegundua taa/bulb za umeme
ikanitia moyo sana. Huyu bwana alifanya
majaribio 10,000 ili aweze kugundua taa
tunazozitumia leo na yote yakafeli. Watu
wakamwambia sasa ni vizuri ukaachana na
hilo jaribio maana umefeli vya kutosha. Huyu
bwana akasema sijafeli ila nimejifunza mara
10,000 jinsi ambavyo fomula zangu hazifanyi
kazi na naedelea kuboresha. Mwishoni
akafanikiwa kugundua taa na kuanzisha
kampuni kubwa sana duniani ya umeme
inayoitwa General Electric Company ambayo
ipo na inazidi kukua hadi leo. Historia ya
huyu bwana inafanana na ya Ford, Honda,
Rais Linkolin wa Marekani na wagunduzi wa
ndege. Hata katika mazingira ya
wafanyabiashara na wafanyakazi wetu
nimekutana na watu waliofilisika, waliopata
hasara, waliofukuzwa kazi, waliofeli shule,
walioshindwa katika mahusiano na
waliokatishwa tamaa sana. Lakini napenda
kuwatia moyo kwa kuzingatia elimu
tunayopata kwa watu waliofanikiwa kuwa;
i) Usikate tamaa, kufeli ndiyo kujifunza mbinu
mpya
ii) Kufeli na kupata hasara ni gharama/ada ya
mafanikio utakayopata baadaye
iii) Kufeli ni nafasi mpya ya kuanza tena,
lakini ukiwa umejipanga vizuri zaidi
iv) Changamoto yeyote usipokuua
inakuimarisha zaidi
v) Usirudi nyuma hata kama changamoto ni
kubwa
vi) Ukiamini unaweza, unaweza na ukiamini
huwezi, huwezi
vii) Kufeli kunakupa shule ambayo hutasahau
daima.
Asanten sana, kwa wote unaosapoti na
kunifanya niendeelee kufanya kazi hii ya
kuelimisha uma wa watanzania kwa ujumla,
shukrani sana,
NakaribishA maoni maoni na ushauri karibun
sana.
Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES