{ google_language = "en"; } { google_language = "en"; } WEKA MAKENGO ~ MAKI INSPIRE

new

new job

http://go.oclasrv.com/afu.php?id=1313272

WEKA MAKENGO


Anza kuwa na malengo, ili akili yako ifanye
kazi vizuri nilazima ijue inafanya kazi kwaajili
gani? Nilazima uiwekee malengo nah ii
itakusaidia sana kuona fursa
zinazokuzunguka. Kama ambavyo huwezi
kwenda chooni bila kubanwa na haja ndivyo
hivyo hivyo huwezi kununua kiwanja au
kufungua biashara kama huna mpoango wa
namna hiyo.
Mipango ndiyo huleta ulazima wa kufanya
baadhi ya mambo. Amua ni kitu gani unataka
kukifanya, kwa mfano unaweza kusema kuwa
mwaka huu nataka kufungua biashara ya kitu
flani, ukishakuwa na wazo hilo tu akili yako
itaanza kuwaza ni vitu gani vinahitajika ili
kuifungua hiyo biashara na vinapatikanaje,
hapo moja kwa moja utakuwa umeijaza akili
yako na mambo chanya.
Lakini bila kuwa na malengo akili yako
inakuwa haifanyi chochote, ipo tu na
haisjishughulishi. Hutaona fursa mpya,
kwanza hutakuwa na haja ya kuzitafuta
kwakuwa huzihitaji, utajikuta matumizi yako
yapo kwenye mambo yasiyo na msingi
kwakuwa huna malengo. Lakini kama una
malengo ya maendeleo sidhani kama utafanya
mambo ya kipuuzi, huwezi kununua
smartphone ya laki tatu wakati una lengo la
kununua kiwanja cha laki tano.
Akili yako yenyewe bila kuiambia itafanya
maamuzi ya kupima kipi cha muhimu kati ya
smartphone ya pili au kiwanja cha kwanza.
Anzia hapo kwa kuwa na malengo, kisha weka
mikakati ya kuyafikia hayo malengo na
utajikuta ni mtu mpya, utaona namna
ambavyo kiasi kidogo unachopata sasa
unaweza kukiwekeza kwa faida na kuacha
kuwa mtu wa kulalamika, watu wote
waliofanikiwa walishaweka mapengo ya
kufanikiwa weka yako sasa.
Akili zetu zimetengenezwa kwa namna
ambayo zinafanyakazi kutokana na malengo
flani. Hii ndiyo maana katika kipindi ha
mitihani wanafunzi huhangaika kusoma sana
kwakuwa kuna mitihani, kusingekuwa na
mitihani akili isingehangaika namna hiyo
kutafuta mbinu za kufaulu. Weka mlaengo ya
kufungua biashara, malengo ya kununua
kiwanja na kufanya uwekezaji wa aina yoyote
ile.
Ukishakuwa na malengo akili yako itaanza
kufanya kazi kuyafikia na utaona namna fursa
zitakavyoonekana, utaona namna
utakavyopunguza matumizi yasiyo na msingi,
utaona namna ambavyo kila shilingi
utakayoipata utaipeleka kwenye mambo ya
maana na kubwa kabisa utaona mabadiliko
katika maisha yako. WEKA MALENGO.

Share:

No comments:

GET LATEST JOBS and VACANCIES UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Get Latest Jobs Vacancies Alert Via Our Facebook Page

LATEST JOBS & VACANCIES