Home »
MOTIVATION AND INSPIRATION ISSUES
» TUNA MIAKA MINGI YA KUZALIWA LAKINI HUTAJAKUWA, NDIO MAANA HATUFANIKIWI
TUNA MIAKA MINGI YA KUZALIWA LAKINI HUTAJAKUWA, NDIO MAANA HATUFANIKIWI
Mara nyingi watu wengi tunapozeeka udhania
kwamba tumekua kumbe ndio kwanza
tunazidi kuwa watoto wachanga. Mafanikio
makubwa yanapatikana kwa urahisi kwa wale
tu waliokua na si waliozeeka. Ukikua ndipo
unapata-
mafanikio, watu wengi hatujafanikiwa
kwasababu hatujakua hata kidogo, japo kuwa
tunakwenda kuzeeka.
Inabidi “kukua”. Watu uzeeka, lakini wawe
wamekua na siyo kuzeeka peke yake. Watu
wengi uishi kwa kutunzwa na kukingwa na
wazazi, wakitoka kwenye kinga ya wazazi
bado wanakwenda kwenye kinga ya kampuni
binafsi, shirika au serikali.
Kwa maneno mengine watu wengi
tunategemea zaidi mtu mwingine kutulinda/
kutujali au mtu mwingine abebe majukumu
yetu kutokana na sisi kukosa busara na akiri
ya msingi nay a kawaida. Ndiyo maana
tunatafuta kwa nguvu zetu zote usalama wa
ajira au kupata hifadhi ya mwajiri.
Watu wengi sana utumia muda wao mwingi
kutafuta dhamana ya maisha na katika
maisha yao yote ujitahidi sana kukwepa
hatari (risks), ambazo wanazohisi zinaweza
kuwapata endapo wakithubutu kufanya
chochote kujikwamua kiuchumi. Pia, wengi
wetu tumekuwa tukikwepa kukua na mara
zote kutafuta wazazi wa kurithishwa, ili
watutunze na kutujali.”
Mimi na wewe tunafahamu watu wengi
ambao hawana uwezo wa kufurukuta bila
mafao ya uzeeni (pension). Tunafahamu,
watu ambao hawajazeeka au kufikia umri wa
kuchukua mafao yao kutoka kwenye mifuko
ya hifadhi ya jamii, lakini ukiongea nao sasa
hivi tayari wameanza kuhesabu kwamba
pension yao na bima za afya vitakuwepo
kuwatunza uzeeni na au siku za mbeleni.
Ukweli ni kwamba kinga au aina hizi za
hifadhi ya jamii zilitengenezwa na kuwekwa
wakati wa zama zile za mapinduzi ya
viwanda huko Ulaya na Marekani. Mifuko ya
hifadhi ya jamii wakati huo iliwekwa kwaajili
ya kutoa kinga kwa wale vibarua maskini wa
viwandani, ambao walikuwa ni wahitaji
kwelikweli. Bahati mbaya leo hii kuna watu
wengi, hasa wale waliosoma na wanalipwa
mishahara mikubwa bado wangali
wakihesabu au wakitegemea waajiri wao
wawatunze na kuwajali.
No comments:
Post a Comment