Ni vizuri kujizoesha kutafakari kuhusu wewe ni
nani, mapungufu yako, mambo gani makubwa
na mazuri uliyokwisha wahi kufanya, na vitu
gani hasa unavipenda na usivyovipenda.
Tafakari hii itakupa picha ya aina gani ya mtu
wewe ulivyo, na kukusaidia kujipanga kuziba
yale mapungufu, na wakati huo huo, utaweza
kuangaza fursa zilizopo na unazoweza
kuzitumia kutokana na 'ubora' ulionao.
Tafakari hii itakuwezesha pia kutambua kitu
kiitwacho kwa kiingereza 'passion', yani
mambo unayoyapendelea sana kufanya au
kuwa hapo baadae. Umuhimu wa kutambua
passion ni kwamba ukiweza kuwekeza muda
katika passion yako inaweza kuwa sehemu
nzuri ya kujijengea maisha yenye furaha.
Kwani passion itakufanya ufanye jambo
utalotaka kulifanya kwa ufanisi na pia hata
ukikumbana na changamoto, hautokata tamaa
kirahisi rahisi.
Home »
MOTIVATION AND INSPIRATION ISSUES
» JIFUNZE KUTAFAKARI KUHUSU WEWE
No comments:
Post a Comment