Wengi huwa tunapenda sana
kusema, “siyo riziki” au
“haikuandikwa” hata pale ambapo
tunafanya makosa ya kukusudia.
Badala ya kujifunza na
kujirekebisha au kutumia makosa
yetu kujifunza, huwa tunajiridhisha
na kujifurahisha kwa kudai tu
kwamba siyo riziki.
Hali hii iko sana pale ambapo
tunashindwa kufikia malengo au
kuanguka katika shughuli au juhudi
za kufikia shughuli fulani. Badala
ya kuchukulia maanguko yetu kama
shule, kama sehemu muhimu ya
kung’amua udhaifu wetu na
kuurekebisha huwa tunachukulia
maanguko yote kama kushindwa.
No comments:
Post a Comment