Mapato ya Ajira . Haya ni mapato yanayotokana na kufanya kazi ya kuajiriwa (mshahara), ambayo mtu huyapata kutokana na ajira yake. Katika aina hii ya kipato, vigezo vya kukuwezesha ulipwe ni pamoja na aina ya kazi na wadhifa au cheo chako. Pia, mapato haya yanajumuisha mapato yoyote yatokanayo na ajira binafsi (kujiajiri), biashara ndogondogo na shughuli nyinginezo ambazo unapata kipato kutokana na juhudi na muda uliotumika. Kwa maana nyingine, ni kwamba kama husiposhugulika au ukasimama kufanya kazi na kipato kinakoma pale pale. Ø Uzuri wa Mapato ya Ajira · Mapato yanaongezeka zaidi kulingana na muda na ukubwa wa shughuli inayofanya · Hauitaji mtaji kuweza kupata mapato haya · Mtaji ni nguvu au ujuzi wako mwenyewe Ø Ubaya wa Mapato ya Ajira · Uwezi kupata utajiri wa kudumu kwa aina hii ya mapato yanayotokana na mshahara. Kwasababu mshahara unapata, unakula na unanaisha.......Unapata unakula zinaisha..... · Siyo mapato endelevu, ukiacha kufanya kazi mapato yanakoma. · Mapato haya ya ajira yanatozwa kodi kubwa kuliko aina nyingine zote za mapato na Waajiriwa wanalijua vizuri hili. Mfano; kwa mtu anayelipwa mshahara wa kiasi cha 1,350,000/- anakatwa kodi hivi: Aina ya Makato Kiasi (TSh)/ Mwezi Kodi (Income Tax) 260,400.00 Bima ya Afya 40,500.00 Chama cha Wafanyakazi 27,000.00 Mfuko wa Pensheni 67,500.00 Jumla 394,900.00 Sasa, ebu fikiria mtu anakatwa karibu Shilingi 400,000/- kila mwezi, kiasi ambacho kwa mwaka kinafikia karibu shilling 4,800,000/-. Unaweza kukuta mtu ana biashara yenye mtaji upatao shilingi million 15, siajabu kukuta analipa kodi kiasi kisichozidi shilingi 500,000/- kwa mwaka. |
No comments:
Post a Comment