Home »
MOTIVATION AND INSPIRATION ISSUES
» INAWEZEKANA WALA USIMSINGIZIE MUNGU KAMA WAFANYAVYO WENGI
INAWEZEKANA WALA USIMSINGIZIE MUNGU KAMA WAFANYAVYO WENGI
Hii inawezekana ndugu zangu na wala msimsingizie mungu kama idadi kubwa inavyoamin na kuasema ,mungu alishaumba ulimwengu na binadamu anachofanya ni kubaririki kazi za mikono yetu , hii inawezekana kwa Kutumia kila fursa ipasavyo,
Fursa ziko kila sehemu, unachohitaji
ni malengo madhubuti unayotaka
kutimiza. Una utashi mkubwa
na vipaji vingi vinavyoweza kutumika
katika kutumia fursa mbalimbali na
kuinua maisha yako. Njia pekee ya
kuanza kufahamu uwezo wako
mkubwa ni kujitambua.
Kujitambua ni kufahamu fursa
unazotaka kuzitumia kuendeleza
maisha kwa kufanya yale muhimu
na kuacha yasiyo na tija kwako,
na niendelee kwa kusema kuwa
Fikra zako zina mchango mkubwa
sana katika kuendesha maisha yako.
Ili kubadili maisha, ni lazima
kubadili fikra. Kubadili fikra ni kitu
cha kwanza na cha msingi.
Ili tuweze kufikia malengo,
tunatakiwa kupanua wigo wa fikra
zetu na kuona mbali zaidi ya leo na
kesho. Hii inawezekana kwa kila
mmoja wetu, ingawa si kazi rahisi.
WENU
ALEX LIMAKI
Kwa elimu zaid ya mafanikio itakayobadili maisha yako endelea kutembelea blog yetu:makinspire.blogspot.com
No comments:
Post a Comment